(SWAHILI) QURAN SURE SEÇİNİZ
|
|
| 1 - AL-FAATIH'A |
| KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
![]() |
| 1. | KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
| 2. | Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote; |
| 3. | Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu; |
| 4. | Mwenye Kumiliki Siku ya Malipo. |
| 5. | Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada. |
| 6. | Tuongoe njia iliyo nyooka, |
| 7. | Njia ya ulio waneemesha, siyo ya walio kasirikiwa, wala walio potea. |
